Waziri wa fedha wa Sudan Bw Mohamed Osman al-Rikabi amesema uchumi wa Sudan unakabiliwa na changamoto, lakini zinatatulika kwa sera na utaratibu.
Bw. Al-Rikabi amesema moja kati ya changamoto hizo ni "kushuka kwa thamani ya paundi ya Sudan" na "kupanda kwa gharama za kununua bidhaa za kimkakati" pia ni suala linalojitokeza.
Pia amesema taabu ya kupata fedha kutokana na tuhuma kuwa Sudan inafadhili ugaidi na urali wa kibiashara ni changamoto nyingine inayoikabili Sudan.
Ameongeza kuwa Sudan bado haijanufaika na uamuzi wa Marekani wa kuiondolea vikwazo mwezi Oktoba mwaka jana, lakini anaona matokeo mazuri ya uamuzi huo yataonekana baada ya muda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |