• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watoto wakimbizi kutoka Syira mjini Istanbul wapewa zawadi za mwaka mpya

    (GMT+08:00) 2018-01-03 09:48:10

    Shirika la hisani la Social Market limewapatia watoto zaidi ya 250 wakimbizi kutoka Syria mjini Istanbul, zawadi za mwaka mpya na kuwaonyesha michezo mbalimbali wakiwa pamoja na familia zao.

    Akizungumza kwenye hafla ya kutoa zawadi hizo, meya wa wilaya ya Beyoglu, Bw Ahmet Misbah Demircan, amesema katika wakati huo mgumu, ni jukumu lao kuwasaidia watoto wa Syria. Habari zinasema, zawadi hizo ni pamoja na nguo za baridi na vifaa vya masomo.

    Shirika la Social Market limeahidi kuzisadia familia 100 za wakimbizi kutoka Syria zenye mapato ya chini. Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wakimbizi kutoka Syria nchini Uturuki imefikia milioni 3.3, laki 5 kati yao wanaishi mjini Istanbul.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako