• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Palestina yailaani Israel kupitisha mswada wa kuimarisha udhibiti wa Jerusalem

    (GMT+08:00) 2018-01-03 09:54:34

    Palestina imelilaani bunge la Israel kupitisha mswada wa sheria inayolenga kuimarisha udhibiti wa Jerusalem, na kuitaja kuwa ni "haramu".

    Msemaji wa Ikulu ya Palestina amesema mswada huo uliopitishwa na bunge la Israel na uamuzi uliotangazwa na rais Donald Trump wa Marekani kuhusu kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, wote ni "haramu", na ni hatua ya kutangaza vita dhidi ya wapalestina.

    Msemaji huyo pia amesisitiza kuwa mipango yoyote ya kisiasa isiyohusisha suala la Jerusalem haitafanikiwa.

    Mswada huo unaagiza kuwa, mabadiliko yoyote yatakayofanywa na serikali ya Israel kuhusu hadhi ya Jerusalem, yanahitaji zaidi ya theluthi mbili ya kura za wabunge. Wachambuzi wanaona hatua hiyo itaimarisha udhibiti wa Israel kwa Jerusalem.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako