• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Ligi Kuu Uingereza: FA yamtaka kocha Wenger kujieleza kuhusu matamshi yake

    (GMT+08:00) 2018-01-03 09:59:21
    Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amefunguliwa mashtaka na Chama cha Soka England (FA) kutokana na tamko lake kuhusu waamuzi timu yake ilipocheza na kupata matokeo ya sare ya 1-1 ugenini dhidi ya West Brom.

    Wenger alikasirika baada ya mwamuzi Mike Dean kuwapa West Brom mkwaju wa penalti, ambapo walifunga na kusawazisha.

    Inadaiwa kwamba, aliyoyafanya Wenger katika chumba cha kubadilishia mavazi cha waamuzi baada ya mechi yalikuwa matusi na ya kukera huku akionyesha kutilia shaka maadili na uwezo wa mwamuzi.

    Kufuatia shitaka hilo, Wenger amepewa nafasi ya kujitetea hadi ifikapo ijumaa saa kumi na mbili za jioni kwa saa za Uingereza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako