• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Ligi Kuu ya Uingereza: Manchester City yaongoza kwa tofauti alama 15 kwenye msimamo

    (GMT+08:00) 2018-01-03 09:59:43
    Klabu vinara wa ligi kuu nchini Uingereza Manchester City, imefanikiwa kuongeza tofauti ya alama na kufikia 15 dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili kufuatia ushindi iliopata jana.

    City wameifunga timu ya Watford magoli 3-1, yaliyopatikana kupitia Raheem Sterling, Christian Kabasele la kujifunga, na Sergio Aguero, hivyo kuifanya timu hiyo ifikishe alama 62 katika mechi 22 ilizocheza mpaka sasa, ikifuatiwa na Manchester United yenya alama 47.

    Katika mechi nyingine zilizofanyika jana, Southampton ilifungwa nyumbani na Crystal Palace kwa magoli 1-2, Swansea ikifungwa na Tottenaham 2-0, na West Ham United wakipata ushindi wa 3-1 dhidi ya West Brom Albion.

    Ligi hiyo inaendelea usiku wa leo, ambapo Arsenal watawakaribisha Chelsea katika pambano la upinzani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako