• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani kuiwekea Pakistan shinikizo zaidi kuhusu kupambana na ugaidi

    (GMT+08:00) 2018-01-03 16:55:41

    Ikulu ya Marekani imeitaka Pakistan iongeze juhudi kupambana na ugaidi, na kusema itatangaza hatua kabambe za kuiwekea Pakistan shinikizo katika saa 24 hadi 48 zijazo.

    Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Bi. Nikki Haley amesema, Marekani itaendelea kusitisha msaada wa kijeshi wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 255 kwa Pakistan. Hivi karibuni, rais Donald Trump wa Marekani ameituhumu Pakistan kwa kutoa hifadhi kwa magaidi, pia amesema hali hiyo lazima ikomeshwe.

    Serikali ya Pakistan imepinga malalamiko hayo ya Marekani, na kusema imesikitishwa na kitendo cha Marekani cha kupuuza mchango wa Pakistan katika kupambana na ugaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako