• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaimarisha usalama katika eneo la mpaka baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kuua askari polisi watano

    (GMT+08:00) 2018-01-03 17:48:05

    Mamlaka nchini Kenya imeimarisha ulinzi katika mpaka wa nchi hiyo na Somalia kwenye kaunti ya Mandera baada ya wapiganaji wa kundi la Al Shabaab kuwaua askari polisi watano jana jioni.

    Mratibu wa mkoa wa Kaskazini mashariki Mohamud Saleh amesema askari polisi hao waliuawa walipokuwa wakifanya doria katika barabara ya Elwak-Kotulo kwenye Kaunti ya Mandera. Amesema askari wengine zaidi wamepelekwa kwenye eneo la tukio, ikiwa ni juhudi za kuwakamata wapiganaji hao ambao wakazi wa eneo hilo wanadai kuwa wameonekana katika eneo hilo wiki chache zilizopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako