• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Mapato ya mauzo ya korosho nchini Tanzania yaongezeka

  (GMT+08:00) 2018-01-03 18:45:43

  Mapato kutokana na mauzo ya korosho nchini Tanzania katika msimu wa 2017/2018 katika mikoa minne ya Lindi, Mtwara, Pwani na Ruvuma, yamepanda na kufi kia Sh trilioni 1.08 ikilinganishwa na misimu miwili iliyopita.

  Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Hassan Jarufu, wakati akifafanua juu ya uzalishaji na mauzo ya zao la korosho nchini hadi kufikia mwisho wa mwaka 2017.

  Korosho inaiingizia Tanzania takribani asilimia 15 za fedha za kigeni.

  Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), kwa Afrika, Tanzania inashika nafasi ya nne kwa uzalishaji wa korosho ikizalisha asilimia 20 ya korosho zote, lakini kwa duniani, inashika nafasi ya nane.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni 10 kwa msimu wa 2017/2018 amesema , Bodi ya korosho inaratibu uzalishaji wa jumla ya miche 14,001,820 ambayo imetokana na tani 100 (kilo 100,000) zilizozalishwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako