• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Watanzania watakiwa kutilia maanani kilimo cha nazi

    (GMT+08:00) 2018-01-03 19:01:35

    Mtafiti kiongozi kutoka Kituo cha Utafi ti wa Kilimo Mikocheni jijini Dar es Salaam, Dk Andrew Ngereza amesema kuwa mafuta ya mwali ya nazi, yanaweza kuwatajirisha Watanzania kwa haraka kutokana na mafuta hayo kuuzwa kwa bei ya juu.

    Dk Ngereza alisema kuwa lita moja ya mafuta hayo, huuzwa hadi Sh 50,000, wakati robo lita (ujazo wa mililita 250) huuzwa kati ya Sh 12,000 hadi Sh 15,000, na hayana kemikali yoyote.

    Alisema mafuta hayo ni moja ya mafuta, yanayouzwa kwa bei ya juu na uhitaji wake katika soko la kimataifa ni mkubwa. Kwa mujibu wa mtafiti huyo, zao la nazi ambalo Tanzania ndiye mzalishaji namba moja Afrika na namba kumi duniani, lina faida nyingi katika maisha ya watu na kuleta ustawi katika mazingira yao.

    Alisema mti wa mnazi, unajulikana kama mti wa uhai kutokana na bidhaa nyingi zinazopatikana katika zao hilo.

    Bidhaa nyingine zinazotokana na zao la nazi ni makuti kwa ajili ya kuezeka nyumba, fagio, vikapu, mbao, samani, sakafu, karatasi na dawa za kufukuza mbu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako