• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Wadau wa sekta ya nafaka Uganda kukutana kujadili bei ya chini ya mahindi

    (GMT+08:00) 2018-01-03 19:04:17

    Wadau katika sekta ya nafaka nchini Uganda watakutana hivi karibuni ili kujadili bei ya chini ya mahindi hasa yanayonunuliwa na wafanyabishara wa nchi nyingine za Afrika Mashriki.

    Mwenyekiti wa baraza la nafaka nchini humo Chris Kaijuka, amesema kushuka kwa bei hiyo ya mahindi kumechangiwa na mavuno mazuri msimu huu.

    Uganda hadi sasa imeuza karibu tani 38,000 za mahindi za thamani ya dola milioni 15 kwa nchi jirani kwa nusu bei ya ile ya kimataifa.

    Rwanda kupitia kwa mipaka ya Gatuna na Cyanika imenunua tani 5,405 ikifuatiwa na DRC ambayo imenunua tani 1,105 kupitia mipaka Rusizi, Mpondwe na Rubavu huku mayo Tanzania ikiagiza tani 480.

    Wafanyabiashara wananunua mahindi kutoka maeneo ya Tororo, Gulu, Masindi na Lira kwa bei ya dola 180 kwa tani moja lakini nchini Kenya tani moja imefikia dola 430.

    Hata hivyo uagiziaji huo wa mahindi kwa bei rahisi kutoka Uganda haujapokelewa vyema na wakulima wa Kenya ambao walitarajia watauza bidhaa yao kwa bei zuri.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako