• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Mauzo ya bidhaa za Kenya Tanzania yapungua

    (GMT+08:00) 2018-01-03 19:04:39

    Mauzo ya bidhaa za Kenya nchini Tanzania katika kipindi cha miezi kumi iliopita yameendelea kushuka huku kukiwa na majibizano ya kibishara kati ya Nairobi na Dar es Salaam.

    Hadi mwezi Oktoba mwaka 2017 kenya iliuza bidhaa za thamani ya dola milioni 227 ikilinganishwa nan dola milioni 280.2 kipindi sawa na hicho mwaka wa 2o16.

    Haya ndio mauzo ya chini zaidi tangu mwaka wa 2007 na ni ishara kwamba biashara kati ya nchi hizo mbili haijakuzwa na kuwepo na makubaliano ya soko la pamoja la jumuiya ya Afrika Mashariki tangu mwkaa 201o.

    Kumekuwa na mzozo kati ya nchi hizo kuhusu maswala kama vile kuondolewa kwa vikwazo vya ushuru na vile vya mpakani hali ambayo imeathiri biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako