• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Leseni za dijitali kutolewa mwezi huu

    (GMT+08:00) 2018-01-03 19:04:58

    Madereva wa magari ya usafiri wa umma wataanza kutumia leseni mpya za dijitali kuanzia mwezi huu.

    Leseni hizo za elektroniki ama e-license zitatolewa kwa madereva wote wa umma kwa shilingi elfu 3 kila mmoja.

    James Macharia waziri wa uchukuzi amesema madereva hao watapewa alama za kufanya kazi vizuri na pia watapokonya alama kwa kusababisha ajali.

    Aidha madereva watakaohusika kwenye makosa mengi ya barabarani watapokonywa leseni na kusimamishwa kufanya kazi.

    Macharia pia ameonya kwamba madereva wa magari ya umma watalazimika kufanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara katika vituo vya kufunza uendeshaji ili kuthibiisha uwezo wao.

    Bodi ya kitaifa ya usalama wa barabarani itatoa maelezo yote ya madereva wanaovunja sheria za barabarani kwa kampuni za bima zitakazowaongezea ada za bima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako