• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa Zambia akabidhi barua ya kujiuzulu kwa rais

    (GMT+08:00) 2018-01-04 08:58:12

    Ikulu ya Zambia imethibitisha kuwa imepokea barua ya kujiuzulu ya waziri wa mambo ya nje Bw Harry Kalaba.

    Msemaji wa rais wa Zambia Bw. Amos Chanda amesema ikulu ya Zambia imetangaza kwamba barua hiyo iliwasilishwa jana usiku. Kabla ya hapo msemaji huyo aliviambia vyombo vya habari kuwa ikulu ya Zambia haijapokea barua rasmi ya kujiuzulu, na waziri huyo bado yupo madarakani.

    Wakati huo huo Bw Harry Kalaba alisisitiza kwenye ukurasa wa facebook kuwa amejiuzulu, na atakabidhi barua. Amemshukuru rais wa Zambia kwa kumpatia nafasi ya kuihudumia serikali yake. Lakini hataachia ubunge kwa kiti cha chama tawala, na ataendelea kuwa mwanachama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako