• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Libya yataka kurejesha uhusiano wa kawaida na nchi za Afrika

    (GMT+08:00) 2018-01-04 09:08:43

    Waziri mkuu wa Libya Bw Fayez Serraj amesema hali inayoboreshwa nchini Libya itachangia kurejeshwa kwa uhusiano wa kawaida kati yake na nchi za Afrika.

    Bw. Serraj ameyasema hayo alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Nigeria Bw. Geoffrey Onyeama, ambapo wamejadili uhusiano na ushirikiano kati ya nchi zao, katika kupambana na uhamiaji haramu, na wamekubaliana kufanya uratibu wa moja kwa moja na wa kupitia Umoja wa Afrika.

    Taarifa iliyotolewa na ofisi ya habari ya waziri mkuu wa Libya, inasema mawaziri hao wamesisitiza umuhimu wa uamuzi uliotolewa kwenye mkutano wa kilele wa Ulaya na Afrika mjini Abidjan, na operesheni ya pamoja ya kuvunja mtandao wa biashara haramu wa binadamu. Pia wamekubaliana kuwarudisha wahamiaji haramu wa Nigeria kutoka Libya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako