• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ethiopia kuwaachia huru wapinzani kama sehemu ya mpango wa msamaha

    (GMT+08:00) 2018-01-04 09:09:32

    Ethiopia imetangaza kuwa itawaachia huru wapinzani walioko gerezani ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa msamaha ili kufikia maafikiano ya kitaifa na kuharakisha demokrasia.

    Taarifa iliyotolewa na waziri mkuu wa Ethiopia Bw Hailemariam Desalegn kupitia ukurasa wa Facebook, imesema gereza la mahabusu la Maekalwi lililoko mjini Addis Ababa litafungwa.

    Taarifa hiyo haijatoa maelezo kuhusu nani watakaoachiwa huru na gereza la mahabusu la Maekalwi litafungwa lini.

    Waungaji mkono wa upinzani na wanaharakati wameilaani serikali ya Ethiopia kulitumia gereza la mahabusu kuwalazimisha watuhumiwa kukiri makosa, haswa wale wanaoshtakiwa chini ya sheria ya kupambana na ugaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako