• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yazalisha tani 100 za dhahabu mwaka 2017

    (GMT+08:00) 2018-01-04 09:40:16

    Wizara ya madini ya Sudan imetangaza kuwa mwaka jana Sudan ilizalisha tani mia moja za dhahabu, zikiwa na thamani ya dola za kimarekani milioni 400. Taarifa iliyotolewa na waziri wa madini wa Sudan Bw. Hashim Ali Salem inasema wizara yake inaendelea na juhudi za kuondoa vizuizi vya uwekezaji kwenye sekta ya uchimbaji wa dhahabu na kupambana na magendo ya madini hayo. Sudan inatafuta kufanya madini ya dhahabu yawe chanzo kikuu cha fedha za kigeni baada ya kupoteza robo tatu ya mapato ya mafuta kutokana na kujitenga kwa Sudan Kusini mwaka 2011.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako