• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi Msumbiji yasema mashambulizi yaliyotokea kaskazini mwa nchi kuwa ni ya kigaidi

    (GMT+08:00) 2018-01-04 09:40:52

    Polisi nchini Msumbiji wametaja mashambulizi yaliyotokea kwenye eneo la pwani la Mocimboa da Praia katika jimbo la Cabo Delgado, kuwa vitendo vya kigaidi, na kusema wahusika watafikishwa mbele ya sheria. Mwezi Oktoba mwaka jana kundi la watu wapatao 30 wenye silaha walifanya mashambulizi kwa wakati mmoja dhidi ya vituo vitatu vya polisi huko Mocimboa da Praia, na kusababisha vifo vya maofisa wawili wa polisi na kiongozi mmoja wa kijamii. Mpaka sasa polisi wamewakamata watuhumiwa 251, lakini pia wamekiri kuwa washambuliaji halisi bado hawajakamatwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako