• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Guinea ya Ikweta yazuia jaribio la mapinduzi

    (GMT+08:00) 2018-01-04 10:03:40

    Wizara ya usalama ya Guinea ya Ikweta imetoa taarifa kuwa, serikali ya nchi hiyo imezuia jaribio la mapinduzi lililopangwa na waasi wa upinzani wenye msimamo mkali, na kutekelezwa na mamluki kutoka nje.

    Taarifa imesema, tarehe 24 mwezi uliopita, mamluki walioajiriwa na baadhi ya waasi wenye siasa kali wa chama cha upinzani, walijipenyeza nchini humo na kujaribu kumshambulia rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa nchi hiyo aliyekuwa anasherehekea sikukuu nyumbani Mongomo.

    Taarifa pia imesema, serikali ya Guinea ya Ikweta imeshirikiana na idara ya usalama ya Cameroon kuwakamata wahusika wengi wa jaribio hilo la mapinduzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako