• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KIKAPU, Rwanda:APR kujipima kwa Patriots kesho

    (GMT+08:00) 2018-01-04 10:34:34
    Wachezaji wa timu ya APR wamewaahidi mashabiki wao kuwa, kwa vyovyote iwezekanavyo watahakikisha wanaibuka na ushindi katika mechi yao ya kesho watakapoumana na mabingwa watetezi wa ligi ya mpira wa kikapu nchini Rwanda The Patriots.

    APR ambao ni mabingwa mwaka 2010, wanatarajiwa kuwa wageni wa Patriots kwenye mechi hiyo itakayofanyika katika uwanja wa Amahoro.

    Lakini kwa upande wao Patriots, wanahitaji alama moja tu ili kuendelea kuwa vinara katika ligi.

    Ligi hiyo itaendelea tena jumamosi kwa mechi mbili ambapo Espoir watacheza na Rusizi lakini IPRC Kusini watacheza na UGB.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako