• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Scott Dann na Jason Puncheon hawatacheza tena msimu huu

    (GMT+08:00) 2018-01-04 10:44:19
    Meneja Roy Hodgson wa Crystal Palace amesema wachezaji wake wawili Scott Dann na Jason Puncheon hawatacheza tena msimu huu baada ya kuumia sana kwenye kano za goti wakimkabili mchezaji nyota wa Manchester City Kevin de Bruyne. Dann ambaye ni nahodha aliondolewa uwanjani kwa machela wakati wa mechi hiyo ambayo ilimalizika kwa sare tasa Jumapili.

    Puncheon aliumia alipomkabili De Bruyne dakika ya mwisho ya mechi.

    Dann na Puncheon wote wawili walipewa kadi za manjano kwa kumchezea visivyo De Bruyne. Hodgson alisema kabla ya mechi hiyo kuanza kwamba ana wasiwasi sana kutokana na majeraha kikosini kwake na kwamba mechi nyingi msimu wa Krismasi zilikuwa mzigo kwa wachezaji wake. Palace walikatiza mbio za City za kushinda mechi 18 mfululizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako