• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, CAF kutoa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mwaka 2017

    (GMT+08:00) 2018-01-04 10:48:10

    Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) leo linatarajiwa kutoa tuzo za mchezaji bora wa Afrika mwaka 2017. Tuzo hizo zitafanyika jijini Accra nchini Ghana ambapo mchezaji mmoja kati ya watatu waliofika fainali atatangazwa mfalme.

    Wachezaji watatu waliotajwa katika orodha ya mwisho ni mshindi wa tuzo hiyo mwaka 2015 Pierre-Emerick Aubameyang raia wa Gabon ambaye anacheza klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani. Wengine ni Sadio Mane wa Senegal na Liverpool pamoja na Mohamed Salah wa Misri na Liverpool. Aubameyang mwenye umri wa miaka 28 aliibuka kinara wa mabao katika ligi kuu ya Ujerumani baada ya kufunga mabao 31 katika mechi 32 alizocheza. Hapewi nafasi kubwa sana ya kushinda kutokana na kushindwa kutoa mchango kwenye timu yake ya taifa ya Gabon ambayo haikufanya vizuri kwenye michuano ya AFCON 2017 iliyofanyika nchini kwao.

    Sadio Mane ameisaidia timu yake ya Senegal kutinga kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi, hivyo anapewa nafasi ya kushinda. Nyota wa Liverpool na Misri Mohamed Salah anaongoza kwa kupewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo hiyo baada ya kuisaidia Misri kufuzu Kombe la Dunia baada ya miaka 25 kupita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako