• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maombi ya hataza kwa mwaka jana nchini China yaongezeka kwa asilimia 14.2

  (GMT+08:00) 2018-01-04 16:41:50

  Maombi ya hataza kwa mwaka jana nchini China yameongezeka kwa asilimia 14.2 na kufikia milioni 1.382, huku nchi hiyo ikisaini makubaliano 52 ya ushirikiano wa kimataifa kuhusu haki miliki.

  Hayo yamesemwa leo na mkurugenzi wa Mamlaka ya Haki Miliki ya China Shen Changyu. Pia amesema mwaka huu, China itazingatia kuinua sifa ya hataza, na kuhimiza sekta ya viwanda ya China ifikie kwenye ngazi ya kati na ya juu katika mnyororo wa thamani duniani. Anasema,

  "Mwaka huu, China itazingatia hataza zenye thamani zaidi, kuhamasisha na kuunga mkono ubunifu wa haki miliki katika teknolojia na elimu ya kisasa zaidi, ili kuandaa hataza zenye thamani kubwa za kimkakati, kuhimiza hataza zaidi za China zifikie viwango vya kimataifa, na kulenga soko la kimataifa."

  Mamlaka ya Haki Miliki ya China imedokeza kuwa mwaka huu, maombi ya hataza yanatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 7.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako