• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Korea Kaskazini yaipigia simu Korea Kusini kupitia njia ya mawasiliano iliyorejeshwa

    (GMT+08:00) 2018-01-04 17:27:09

    Wizara ya Muungano ya Korea Kusini imesema hakuna majadiliano maalum yaliyofanyika na Korea Kaskazini kupitia mawasiliano ya simu yaliyorejeshwa hivi karibuni katika kijiji cha Panmunjom.

    Korea Kusini na Korea Kaskazini zimefungua tena mawasiliano ya simu hapo jana, hivyo kurejesha mawasiliano hayo ya moja kwa moja kati ya nchi hizo mbili baada ya miaka miwili.

    Wizara hiyo imeongeza kuwa jana Korea Kaskazini iliipigia simu Korea Kusini ili kuchunguza kama simu hiyo inafanya kazi.

    Wakati huohuo, China imepongeza juhudi zinazofanywa hivi karibuni na Korea Kaskazini na Korea Kusini, na inatarajia jumuiya ya kimataifa kuunga mkono juhudi hizo na kuhamasisha pande zote husika zitoe mchango katika kutuliza mvutano na kuongeza hali ya kuaminiana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako