• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya watu 30 wauawa katika mashambulizi yaliyofanywa na waasi Sudan Kusini tangu mwaka huu uanze

    (GMT+08:00) 2018-01-04 18:12:19

    Zaidi ya watu 30 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na waasi katika maeneo yanayodhibitiwa na serikali nchini Sudan Kusini tangu mwaka huu uanze, ikiwa ni mwendelezo wa kukiuka makubaliano ya kusimamisha mapigano yaliyosainiwa na pande zinazopambana mwezi uliopita.

    Msemaji wa jeshi la SPLA Lul Ruai Koang amesema, mashambulizi hayo yanayofanywa na waasi wanaomtii aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar na wale wanaohusiana na aliyekuwa naibu mkuu wa jeshi, Thomas Cirilo, yamesababisha vifo vya watu sita kusini mwa nchi hiyo hapo jana. Amesema watu wengine 24 waliuawa katika mashambulizi kama hayo kwenye mkoa wa Liech, kaskazini mwa Sudan Kusini kuanzia mwanzo wa mwaka huu.

    Kundi kuu la upinzani nchini humo, SPLA-IO limekana kuwa limekiuka makubaliano ya kusimamisha mapigano, na kusema imeunda timu yake kufuatilia makubaliano hayo tete.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako