• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kujenga taasisi ya pamoja na chuo kikuu cha Morocco

    (GMT+08:00) 2018-01-04 18:23:23

    Wizara ya elimu ya China hivi karibuni imepitisha ujenzi wa taasisi ya pamoja itakayojengwa na Chuo kikuu cha Ningxia cha China na Chuo kikuu cha Hassan 1 cha Morocco.

    Chuo Kikuu cha Ningxia kimesema, ujumbe wake ulitembelea chuo kikuu cha Hassan 1 mwezi Novemba mwaka jana, na vyuo vikuu hivyo vimesaini makubaliano ya kuanzisha taasisi ya pamoja ambayo itazingatia utafiti wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kuhudumia biashara na ushirkiano kati ya China na Morocco, na kuimarisha ushirikiano wa elimu ya juu kati ya pande hizo mbili.

    Vyuo vikuu hivyo viwili vitafanya mikutano ya kimataifa, kushirikiana katika kufanya utafiti, pamoja na kufanya ziara za wasomi, mpango wa kubadilishana wanafunzi, utafiti wa maofisa na utoaji mafunzo.

    Kamati ya taasisi hiyo itaundwa na wasomi wa China na Morocco.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako