• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel yashambulia kituo muhimu cha kijeshi katika ukanda wa Gaza

    (GMT+08:00) 2018-01-04 18:23:46

    Jeshi la Israel jana usiku limefanya shambulizi la ndege za kivita dhidi ya kituo kikuu cha kijeshi huko Gaza ili kulipiza kisasi kwa shambulizi la mizinga lililofanywa siku moja kabla.

    Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa jeshi la Israel imesema, ndege hizo zililenga jengo muhimu la kigaidi huko Gaza, lakini hajaeleza hali ya jengo hilo na mmiliki wake.

    Shambulizi hilo limefanywa baada ya mizinga mitatu kupigwa kutoka Ukanda wa Gaza dhidi ya kusini mwa Israel ambayo haikusababisha majeruhi au hasara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako