• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Benki kadhaa zafungwa Tanzania kwa kukosa mtaji

    (GMT+08:00) 2018-01-04 18:40:07

    Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imezifunga na kuzifutia leseni za huduma za kibenki na kuwekwa chini ya mufilisi benki za Convenant Bank for Women (Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera Farmers' Cooperative Bank Limited na Meru Community Bank Limited.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Alhamisi na BOT, hatua hii imetokana na benki hizo kufilisika na hivyo kwenda kinyume na Sheria ya Mabenki na Taasisi za Kifedha ya mwaka 2006.

    Upungufu huo wa mtaji unahatarisha usalama wa sekta ya fedha na kwamba kuendelea kutoa huduma za kibenki kwa benki hizo kunahatarisha usalama wa amana za wateja wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako