• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Wenye biashara ndogo Uganda kunufaika na wakfu wa Tony Elumelu

    (GMT+08:00) 2018-01-04 18:42:11

    Biashara ndogo na zile za wasatani nchini Uganda zinatarajia kunufaika na ruzuku ya shilingi bilioni 360 kutoka kwa wakfu wa Tony Elumelu.

    Mpango wa kutoa ruzuku wa wakfu huo ambao sasa uko kwenye mwaka wa nne umeanza kupokea maombi ya mawazo ya kibiashara ambazo zinaweza kuleta mabadiliko barani Afrika.

    Chini ya mpango huo wanaofaidika watapewa hadi dola 5,000 kama mtaji kwa biashara zao na pia kupata mafunzo kwa wiki 12.

    Mwanzilishi wa wakfu huo Tony O. Elumelu, amesema lengo lake ni kuleta athari za kimaendeleo barani Afrika na kusaidia vijana kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako