• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Waganda wanaoishi nje ya nchi watakiwa kuwekeza nyumbani

    (GMT+08:00) 2018-01-04 18:42:34

    Raia wa Uganda wanaoishi nje ya nchi wametakiwa kuwekeza nyumbani.

    Kulinganga na takwimu za benki kuu ya Uganda, pesa wanazotuma nyumbani raia waishio nje zinafikia zaidi ya dola bilioni 1 ambazo ni nyingi kuliko zile za missada ya wafadhili ambazo ni dola milioni 600.

    Pesa wanazotuma nyumbani Waganda zinaongezeka kwa asilimia 21 kwa miaka 5 iliopita na wataalam nchini humo wanasema kukiwa na mpango mzuri zinaweza kusaidia pakubwa kukuza uchumi wa kitaifa.

    Akizungumza na baadhi ya waganda wnaoishi nje ya nchi mjini Kampala naibu mkuu wa benki kuu anayeshughulikia ukuaji wa soko la kifedha Arnold Babugwagye, alisema watunga sera wanafaa kuandaa mpango wa kuwezesha fedha hizo kuingia moja kwa moja kwenye uwekezaji wa ndani ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako