• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Putin asaini amri ya kurejesha safari za ndege za moja kwa moja kati ya Moscow na Cairo

    (GMT+08:00) 2018-01-05 08:47:31

    Rais Vladimir Putin wa Russia amesaini amri ya kurejesha safari za ndege za moja kwa moja kati ya miji ya Moscow na Cairo, lakini safari za ndege kati ya Russia na maeneo mengine nchini Misri bado hazijarejeshwa. Mwaka 2015 rais Putin aliamuru kusitisha safari zote za ndege kati ya Russia na Misri, baada ya ndege ya abiria ya Shirika moja la ndege la Russia iliyokuwa inaelekea St. Petersburg kutoka Sharm el Sheikh, kuanguka muda mfupi mara baada ya kuruka kwenye peninsula ya Sinai, na kusababisha vifo vya watu wote 224 waliokuwa kwenye ndege hiyo, wengi wao wakiwa ni raia wa Russia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako