• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Afrika ya Kati yalaani vurugu zilizotokea nchini humo

    (GMT+08:00) 2018-01-05 08:52:49

    Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imelaani vikali vurugu zilizosababisha vifo na kufanya wakazi kukimbia makazi yao kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

    Kwa mujibu wa ripoti ya awali, wapiganaji wa kundi la Revolution Justice wameshambulia makazi ya waislamu mjini Paoua katika mkesha wa mwaka mpya. Naibu msemaji wa Umoja wa mataifa Bw. Farhan Haq amesema, kutokana na jitihada za walinzi wa amani wa Umoja huo, hali ya mvutano kwenye eneo hilo imepungua katika siku iliyofuata.

    Bw. Haq pia amesema, tume hiyo imeongeza nguvu na kuimarisha doria mjini humo ili kuzuia mashambulizi dhidi ya raia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako