• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yakaribisha watalii 576 katika safari ya kwanza ya meli ya kitalii mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2018-01-05 09:27:28

    Kenya iliwalipokea watalii 576 jana kwenye meli ya kitalii MS Nautica ambayo imefanya safari yake ya kwanza mwaka huu.

    Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya utalii wa Kenya KTB Bibi Betty Radier, amesema meli hiyo iliwasili Mombasa kutoka Zanzibar na kutarajiwa kuwepo huko kwa siku moja kabla ya kwenda kisiwa cha Mahe nchini Shelisheli.

    Bibi Radier amesema kuwasili kwa meli hiyo ya kitalii ni msukumo mkubwa kwa sekta ya utalii kwenye sehemu ya pwani nchini humo, na kwamba Serikali ya Kenya imeahidi kuendeleza utalii wa meli badala ya kutegemea tu sehemu ya pwani na safari kwenye hifadhi za wanyamapori.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako