• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikapu NBA: Cavaliers yafungwa na Celtics, Warriors wanusurika

    (GMT+08:00) 2018-01-05 10:15:26
    Licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Dallas Mavericks kwenye mechi ya jana, mabingwa watetezi wa ligi kuu ya kikapu nchini Marekani Golden State Warriors wamafanikiwa kushinda kwa alama 125-122.

    Kwa kile kilichokuwa kikionekana kama Mavericks wanashinda baada ya kuongoza kwa alama katika robo ya pili na robo ya tatu (yaani 35-32, 28-24), mambo yalibadilika katika robo ya nne baada Warriors kujukusanyia alama 34-33.

    Lakini kiama kiliwafika mabingwa wa mwaka 2016 Claveland Cavaliers walipofungwa na Boston Celtics kwa alama 102-88 na kuendelea kuiweka timu hiyo katika nafasi mbaya kwenye msimamo wa ligi.

    Nyota wa Boston waliofanikisha ushindi huo ni Jaylen Brown, Al Horford na Jayson Tatum ambao kwa pamoja walifunga alama tatu kwa wingi kila mmoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako