• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sura ya China duniani inaboreshwa

  (GMT+08:00) 2018-01-05 16:48:24

  Ripoti kuhusu sura ya taifa la China kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka 2017 iliyotolewa na Taasisi ya Utafiti wa China na Dunia katika Karne hii imeonesha kuwa sura ya China imeboreshwa hatua kwa hatua.

  Naibu mkurugenzi wa kituo cha elimu ya mawasiliano na nje katika Idara ya Uchapishaji ya Lugha za Kigeni ya China Yu Yunquan amesema, ripoti hiyo imetolewa kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa katika mataifa 22 duniani na kuwahoji watu elfu 11, na kwamba sura ya taifa la China ilipata alama 6.22, na kudumisha mwelekeo wa kuongezeka hatua kwa hatua unaoonekana katika miaka ya hivi karibuni.

  "Kwa ujumla, sura ya taifa la China duniani imeboreshwa na hata kati ya waliohojiwa, watu walio na maoni mazuri na sura ya China wamefikia karibu asilimia 70 baada ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China. Vilevile Shughuli za kutawala nchi na kushughulikia mambo ya siasa nchini China pia zimepongezwa na watu wa ndani ya nje ya nchi."

  Ripoti hiyo pia imeonesha kuwa ushawishi wa kimataifa wa uchumi wa China umeongezeka na kushika nafasi ya pili duniani na uwezo wa China katika ubunifu wa teknolojia pia umepongezwa

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako