• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Sudan laongeza tena muda wa kusimamisha vita kwa miezi mitatu kwa upande mmoja

    (GMT+08:00) 2018-01-05 18:10:20

    Rais Omar al-Bashir wa Sudan amesaini amri kutangaza jeshi la serikali kuongeza tena muda wa kusimamisha vita kwa upande mmoja kwenye sehemu zote zenye mapigano.

    Lengo la kuongeza tena muda huo ni kujenga mazingira yenye amani kwa mazungumzo ya majimbo ya Kordofan Kusini na Blue Nile, ili kutimiza amani na uvulivu nchini Sudan haraka iwezekanavyo, na kuweka kipaumbele cha kazi ya nchi hiyo katika masuala ya maendeleo yanayotakiwa kutatuliwa.

    Mwaka 2011, jeshi la serikali ya Sudan lilianza kupigana na kundi la upinzani la SPLM-Kaskazini, na tangu mwezi wa Januari mwaka 2014, rais al-Bashir alizindua mchakato wa mazungumzo ya kitaifa, ili kutatua mapigano ya kutumia silaha yaliyodumu kwa muda mrefu na kutimiza amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako