• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania:benki kuu ya Tanzania yafunga biashara za benki 5

  (GMT+08:00) 2018-01-05 18:22:27

  Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imezifungia benki tano kuendesha shughuli zake nchini humo baada ya kubainika kufi lisika.

  Gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu amezitaja benki zilizofungwa kuwa ni Covenant Bank for Women (Tanzania) Limited, Efatha Bank Limited, Njombe Community Bank Limited, Kagera Farmers' Co-operative Bank Limited na Meru Community Bank Limited.

  Gavana Ndulu amesema kuwa BoT itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika benki kwa lengo la kuleta uhimilivu katika sekta ya fedha nchini.

  Alisema katika kuhakikisha usalama wa fedha za wateja wa benki hizo, BoT imeiteua Bodi ya Bima ya Amana kuwa Mfilisi wa benki hizo tano na kuwataka wateja wanaotumia huduma za benki hizo kuwa wavumilivu kwa sasa.

  Mwaka 2012,Benki Kuu ya Tanzania iliongeza kiwango cha chini cha mtaji wa benki za wananchi, Community Banks, kuwa Sh bilioni mbili. Alisema, benki hizo pia zilipewa muda wa miaka mitano kuhakikisha kuwa zinaongeza mtaji kufikia kiwango kipya, muda ulioisha Juni 2017.

  Alisema kuwa kutokana na kushindwa kukidhi Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, BoT imeamua kuzifunga, kusitisha shughuli zake zote za kibenki, kufuta leseni zake za biashara ya kibenki pamoja na kuziweka chini ya ufilisi benki hizo tano kuanzia hiyo jana. BoT imeiteua Benki ya Amana kuwa mfilisi wa benki hizo tano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako