• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya :Biashara za mboga na chakula Zapata hasara kufuatia marufuku ya safari za usiku

    (GMT+08:00) 2018-01-05 18:23:11

    Wafanyibiashara wengi wameshindwa kufika mjini kama ilivyopangwa hasa wale waliodhamiria kusafiri usiku kwa mabasi kutoka sehemu mbali mbali za nchi.

    Hii inafuatia uamuzi wa halmashauri ya taifa ya uchukuzi na usalama barabarani siku ya Jumapili wa kupiga marufuku kwa muda usiojulikana safari za usiku za magari ya uchukuzi wa abiria kufuatia kuongezeka kwa maafa ya ajali za barabarani.

    Jana usiku wasafiri wengi, baadhi yao wakiwa wafanyibiashara waliotarajia kusafiri kote nchini kufikisha bidhaa zao , walikwama katika vituo mbali mbali vya mabasi huku marufuku hiyo ya safari za usiku za magari ya uchukuzi wa umma ikiendelea kutekelezwa.

    Wamiliki wa magari ya uchukuzi wa umma sasa wanalalamika kwamba wamelazimika kukabiliana na changamoto mbali mbali kutokana na marufuku hiyo ya safari za usiku wakisema wanapata hasara kwani wasafiri wanawalazimu kuwapa usafiri mbadala.

    Wafanyibiashara wanaosafiri kutoka Nairobi kuelekea Kampla ni miongoni mwa walioathirika pakubwa na marufuku hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako