• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Baadhi ya wafanyibiashara Uganda walalama faida chache msimu wa likizo

    (GMT+08:00) 2018-01-05 18:23:47

    Baadhi ya wafanyibiashara nchini Uganda wanadai kwamba msimu wa krismasi na mwaka mpya uliokamilika hivi karibuni haukuwaletea faida kama ilivyotarajiwa.

    Wakiongea na vyombo vya habari baadhi yao wanasema krismasi ya mwaka 2017 imekuwa mbaya zaidi katika biashara ikilinganishwa na zile zilizopita.

    Mathius Matesa muuzaji wa viatu katika duka la jumla jijini Kampala amesema mauzo yalipungua kwa asilimia 50 mwaka huu.

    Wataaklamu wa masuala ya mauzo na biashara wa Uganda wameelkeza vidole vya lawama kwa kudodrora kwa uchumi mwaka 2017 kama sababu kuu ya kupungua kwa biashara msimu wa sherehe za mwaka mpya.

    Kwa jumla Uganda ilishindwa kufikia malengo yake ya ukuwaji wa uchumi mwaka 2017 huku idadi kubwa ya watu ikiendelea kusota bila ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako