• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda:Serikali kubinafsisha kiwanda cha viazi cha Nyabihu

    (GMT+08:00) 2018-01-05 18:24:13

    Serikali ya Rwanda inafanya mikakati ya kubinafsisha kiwanda cha usindikaji viazi cha Nyabihu.

    Hatua hii inajiri kufuatia kuporomoka kwa uzalishaji wa bidhaa hiyo na kudorora kwa soko lake.

    Uamuzi huo umeafikiwa katika harakati za kuimarisha kiwanda hicho na kuongeza mapato kwa serikali.

    Wahudumu wana imani kwamba iwapo kiwanda hicho kitapata usimamizi upya ,huenda kikasindika tani sita kwa siku ambapo kwa sasa ilikuwa imefikia tani 2 tu kwa wiki.

    Kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha na kusindika viazi aina nyingi.

    Katibu mkuu wa kiwanda hicho James Ngabo amesema wanatarajia kuwapatia soko la tayari wakulima walioshindwa kuuza viazi vyao baada ya kusimaishwa kwa shughuli za kiwanda hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako