• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zimbabwe asema hataunda serikali ya muungano na chama cha upinzani

    (GMT+08:00) 2018-01-06 18:09:47

    Rais wa Zimbabwe Emerson Mnangagwa ijumaa hii amesema hataunda serikali ya muungano na chama cha upinzani cha MDC-T.

    Hayo ameyasema alipomtembelea ili kumjulia hali kutokana na maradhi ya saratani yanayomsumbua kiongozi wa MDC-T ambaye pia ni waziri mkuu wa zamani wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai katika makazi yake mjini Harare.

    Rais huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa Zimbabwe ni nchi ya Kidemokrasia, hivyo haoni sababu ya kuunda serikali ya umoja na chama cha MDC-T.

    Katika mkutano huo na Tsvangirai, Rais Mnangagwa pia alikutana na mmoja ya makamu watatu wa mwenyekiti wa MDC-T aitwaye Nelson Chamisa ambaye alimpongeza rais Mnangagwa kwa ziara hiyo.

    Morgan Tsvangirai alihudumu kama waziri mkuu wa serikali ya rais wa zamani wa nchi hiyo katika serikali ya muungano kuanzia mwaka 2009 hadi 2013.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako