• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yakanusha kuwepo mgogoro kati yake na Eritrea baada ya kusambaza vikosi vyake katika eneo la mpakani

    (GMT+08:00) 2018-01-06 18:13:35

    Sudan imesema kuwa imesambaza maelfu ya wanajeshi wake katika jimbo la Kassala mashariki ya Sudan ili kupambana na biashara haramu ya kusafirisha binadamu, na hakuna mgogoro kati yake na Eritrea, taarifa hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la SUNA.

    Maelfu ya wanajeshi wa kikosi maalum cha dharura, ambacho ni sehemu ya jeshi la Sudan, wamewasili katika mji wa Kassala ambao upo mpakani mwa Sudan na Eritrea.

    Gavana wa jimbo la Kassala Adam Jamma amesema vikosi vimewasili kufuatia mfumo wa kukabiliana na matukio ya dharura na ikiwa ni agizo la jamhuri la kukusanya silaha na magari yasiyosajiliwa, mbali ya kupambana na biashara haramu ya kusafirisha binadamu na biashara ya magendo ya silaha na bidhaa.

    Gavana huyo pia amekanusha vikali taarifa zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa kuna mpango wa kufunga safari za mpakani mwa Sudan na Eritrea.

    Disemba 30 mwaka 2017, rais wa Sudan Omar al Bashir alitangaza hali ya hatari katika jimbo la Kordofan Kaskazini lililopo magharibi ya Sudan na Kassala la mashariki ya Sudan, hali ambayo itadumu kwa muda wa miezi sita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako