• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yasifu mchango wa China katika sekta yake ya afya

    (GMT+08:00) 2018-01-06 18:16:25

    Sudan Kusini ijumaa hii imeisifu China kutokana na misaada yake ya kifedha na kiufundi katika sekta ya afya kwa taifa hilo la Afrika Mashariki lililoathiriwa na vita.

    Waziri wa Afya Bw. Riek Gai Kok amesema ushirikiano katika masuala ya afya kati ya Sudan Kusini na China tangu miaka sita iliyopita umekuwa na faida kubwa kwa sekta ya afya katika taifa la Sudan Kusini.

    Kwa mujibu wa waziri huyo, China ndiyo mfadhili mkuu wa Sudan Kusini wa vifaa tiba, misaada na mbia mkubwa katika kuwajengea uwezo wataalam wa afya wa Sudan Kusini.

    Msaada wa takribani dola milioni 33 za kimarekani uliotolewa na serikali ya China mwaka 2013 ili kuboresha na kupanua miundo mbinu ya afya katika taifa hilo umesaidia sana kuboresha huduma za afya nchini Sudan Kusini.

    Naye mkuu wa masuala ya Uchumi na Biashara katika ubalozi wa China nchini Sudan Kusini, Zhang Yi, amesema China imejitolea kuendeleza sekta ya afya ya Sudan Kusini kwa kutoa misaada ya kifedha na kwa kuwajengea uwezo wataalam wa sekta ya afya.

    Katika hatua nyingine, Zhang amewasihi watu wa Sudan kutunza amani ili maendeleo yafanyike katika nchi yao iliyoathiriwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka minne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako