• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema hairuhusu wachina na makampuni ya China kujihusisha na masuala yanayokiuka maazimio ya baraza la usalama

  (GMT+08:00) 2018-01-06 18:20:46

  Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika tarehe 5 kwenye wizara ya mambo ya nje ya China, mwandishi mmoja wa habari aliuliza swali akitaka kujua maoni ya serikali ya China kuhusu suala la vyombo vya habari vya Korea Kusini kutoa habari kuwa kuna meli ya kampuni la China ilibadilisha bendera ya nchi ya meli na sehemu ya kujiandikisha, na kisha kujihusisha na mambo yaliyokiuka azimio la baraza la usalama kuhusu kuiwekea vikwazo Korea Kaskazini.

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang alijibu kwa kusema kuwa serikali ya China siku zote inashikilia sera ya kutekeleza azimio la baraza la usalama kwa pande zote, ikitekeleza wajibu wa kimataifa na hairuhusu wachina na makampuni ya China kushughulikia mambo yanayokiuka maazimio ya baraza la usalama.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako