• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za kiarabu kuendelea kususia uamuzi wa Marekani kuhusu hadhi ya Jerusalem

    (GMT+08:00) 2018-01-07 17:39:22

    Mawaziri wa nchi sita za kiarabu pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu jana wamefanya mkutano huko Amman, mji mkuu wa Jordan, wakisisitiza kususia na kupinga uamuzi wa Marekani wa kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, na kusema nchi za kiarabu zitashikilia msimamo wao kuhusu suala la Jerusalem.

    Nchi hizo sita ni pamoja na Jordan, Palestina, Saudi Arabia, Misri, Falme za Kiarabu na Morocco.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiarabu Ahmad Abdoul Gheit amesema, nchi za kiarabu zinashikamana, na wajumbe waliohudhuria mkutano huo wameamua kuendelea kushikilia msimamo wa kususia uamuzi huo.

    Rais Donald Trump wa Marekani mwezi Desemba mwaka jana alitangaza kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, na Marekani itaanzisha mchakato wa kuhamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem. Uamuzi huo umepingwa na jumuiya ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako