• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu 32 hawajulikani waliko baada ya meli mbili kugongana karibu na pwani ya mashariki ya China

  (GMT+08:00) 2018-01-07 18:00:29

  Wafanyakazi 32, wakiwemo wairan 30 na wawili kutoka Bengal, hawajulikani waliko baada ya meli mbili kugongana karibu na pwani ya mashariki ya China jana jumamosi, taarifa hii ni kwa mujibu wa wizara ya Usafirishaji ya China.

  Taarifa ya wizara hiyo, imeeleza kuwa, Mgongano huo, kati ya Meli ya mafuta ya Panama na meli ya mizigo ya kutoka Hong Kong, umetokea majira ya saa mbili usiku ndani ya maji umbali wa maili 160 mashariki ya mlango bahari wa mto Yangtze.

  Wafanyakazi 32 waliopotea walikuwamo katika meli ya mafuta. Na wafanyakazi 21 ambao wote ni raia wa China walikuwa kwenye meli ya mizigo na taarifa zinasema kuwa, wote wameokolewa.

  Mamlaka ya usafirishaji kwa njia ya bahari kutoka China, imepeleka meli nane kwa ajili ya kuwatafuta waliopotea ili kuwaokoa. Na baada ya kuwasiliana na mamlaka ya China ya uokozi, Jamhuri ya Korea imetoa meli ya uokozi na ndege ili kusaidia kuwatafuta.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako