• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan yafunga rasmi mpaka wake na Eritrea ulioko mashariki

    (GMT+08:00) 2018-01-07 18:03:28

    Jana jumamosi Sudan imetangaza rasmi kufunga mpaka wake na Eritrea baada ya kusambaza maelfu ya wanajeshi wake katika jimbo la Kassala lililopo katika mpaka wa Eritrea, shirika la habari la SUNA limeeleza hayo.

    Gavan wa jimbo la Kassala, Adam Jamma ameagiza kufungwa kwa mipaka yote na Eritrea, ikiwa ni utekelezaji wa tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Sudan hivi karibuni katika jimbo hilo.

    Uamuzi huo umeweka sharti la kufungwa mipaka yote na Eritrea kuanzia jioni ya Januari 5 mwaka 2018 hadi taarifa zaidi itakapotolewa.

    Uamuzi huo unakuja saa chache baada ya Serikali ya Sudan kukanusha kuwepo kwa mgogoro baina yake na Eritrea, na kusema kuwa imesambaza vikosi vyake katika jimbo la Kassala ikiwa ni sehemu ya kutekeleza mfumo wake wa dharura na agizo la kukusanya silaha na magari yasiyosajiliwa, licha ya kupambana na biashara harammu ya usafirishaji wa binadamu na magendo ya silaha na bidhaa.

    Disemba 30 mwaka 2017, Rais wa Sudan Omar al Bashir alitangaza hali ya hatari katika jimbo la Kordofan Kaskazini lililoko Magahribi ya Sudan na jimbo la Kassala lililopo Mashariki ya Sudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako