• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa azungumzia mgogoro wa Sahara Magharibi

    (GMT+08:00) 2018-01-07 18:06:47

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, jana jumamosi ameuzungumzia kuongezeka kwa mgogoro katika eneo la Sahara Magharibi na akiitisha kurejeshwa kwa amani katika eneo hilo.

    Katibu mkuu huyo, ameeleza kusikitishwa sana na migogoro iliyozuka hivi karibuni katika eneo la karibu na Guerguerat kwenye ukanda wa kusini wa Sahara Magharibi katika eneo la mpaka wa Morocco na Mauritania.

    Katika maneno yake ya kuhitimisha, katibi mkuu huyo amesema kuondoka kwa utawala wa Polisario katika eneo la Guerguerat mwezi April mwaka 2017, pamoja na tangazo la awali la Morocco kujiondoa katika eneo hilo, lilikuwa jambo muhimu sana lililotengeza mazingira wezeshi ya kufungua majadiliano ya wajumbe wa Umoja wa Mataifa chini ya mwenye heri Horst Kohler.

    Sahara Magharibi ilimegwa kutoka ardhi ya Morcco na Mauritania mwishoni mwa ukoloni wa kihispaniola mwaka 1976. Morocco imelitawala eneo hilo lote tangu 1979, baada ya Mauritania, kwa kuogopa wapiganaji wa Polisario, kuachia eneo lao. Vita ilizuka baina ya Morocco na Chama cha Polisario, ambacho kinapigania uhuru wa Sahara Magharibi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako