• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Donald Trump wa Marekani atoa mapendekezo kuhusu mazungumzo na Bw. Kim Jong-un wa Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-01-07 18:09:57

    Rais Donald Trump wa Marekani, jana tarehe 6 alisema kuwa angependa kufanya mazungumzo yenye masharti na kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong-un.

    Pia amependekeza kuwa, mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini yatakayofanyika tarehe 9 yawe zaidi ya kujadili michezo ya Olimpiki.

    Rais Trump akiwa katika makazi ya rais huko Camp David kwenye jimbo la Maryland aliwaambia waandishi wa habari kuwa anaweza kuwasiliana na Bw. Kim Jong-un kwa njia ya simu, lakini masharti yatawekwa, licha kuwa alimweleza kwamba msimamo wa Marekani kwa Korea Kaskazini ni dhabiti.

    Rais Trump alisema kuwa anaunga mkono mazungumzo kati ya Korea Kaskaini na Korea Kusini yatakayofanyika tarehe 9. Mazungumzo hayo yatahusu kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali, likiwemo suala la Korea Kasazini kujiunga na michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Pyeongchang.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako