• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtu mmoja auawa kwenye maandamano katika jimbo la Darfur magharibi Sudan

    (GMT+08:00) 2018-01-08 08:56:38

    Mwanafunzi mmoja ameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa wakati walipokuwa wanashiriki kwenye maandamano yaliyotokea jana kupinga kuongezeka kwa bei ya mkate huko El Geneina, mji mkuu wa jimbo la Darfur magharibi nchini Sudan. Gavana wa jimbo hilo Bw. Fadl Almula Alhaja amethibitisha kutokea kwa kifo na majeruhi, na kusema maandamano yalifanywa na wanafunzi wa shule binafsi, na uchunguzi utafanyika kuhusu tukio hilo. Mashuhuda wamesema polisi walikabiliana na wanafunzi walioandamana na kusababisha kifo na majeruhi hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako