• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Misri yalaani ripoti ya New York Times kuhusu Misri kukubali uamuzi wa Trump juu ya Jerusalem

    (GMT+08:00) 2018-01-08 09:10:34

    Misri imelaani ripoti ya gazeti New York Times la Marekani kuhusu Misri kukubali uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani wa kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

    Ripoti hiyo iliandikwa na mwandishi wa habari wa New York Times mjini London, akidai kuwa amepata rekodi ya mazungumzo ya simu kati ya ofisa wa ujasusi wa Misri na waendeshaji wa maonyesho ya televisheni ya Misri.

    Katika rekodi hiyo, ofisa wa Misri aliwataka watu mashuhuri nchini humo wakiwemo waendeshaji wa televisheni, kuwashawishi watazamaji wao kukubali uamuzi wa Trump kuhusu Jerusalem.

    Idara ya habari ya Misri SIS imetoa taarifa ikikanusha habari hiyo na kusisitiza kuwa msimamo wa Misri kuhusu suala la Jerusalem utatangazwa na rais, waziri wa mambo ya nje na taarifa ya serikali ya Misri, wala sio kwa njia isiyojulikana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako